KUOMBEA MAZINGIRA YASIZUIE BARAKA ZAKO

| Makala

MAOMBI YA KUOMBEA MAZINGIRA YAKO:

     {Ili yasikwamishe kufanikiwa kwako}

Kuna uhusiano mkubwa sana wa kufanikiwa kwako na mazingira uliyonayo au yanayokuzunguka.ile tu kwamba haujayafahamu haya maarifa haimaanishi utapata msamaha na kusaidiwa kufanikiwa tu.

Kama kweli Mungu anaweza kumfanikisha mtu wake mahali popote pale,basi ni wazi kabisa asingepoteza muda wake kuwahamisha baadhi ya watumishi wake na kwenda kuwabariki kwingine kama ambavyo tunawasoma kwenye biblia…Mwanzo 12:1-2 

“BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka”

Haimaanishi kuwa Mungu hana uwezo wa kukufanikisha popote ulipo,HAPANA, ninachomaanisha ni kwamba, kila mtu amewekewa kitu cha thamani ambacho kinawafaa watu fulani kwa mazingira fulani, na huenda sio kila mtu ataheshimu kile ulichonacho,ila kuna mahali ukikitambulisha kitu chako lazima kitathaminika na kukupa heshima haraka sana, jifunze kitu kwa mfano wa Yusufu…..

Kijana Yusufu sawasawa na maandiko kwenye kitabu cha mwanzo sura ya 37 yote,kuna vitu ambavyo nataka uvione hapo. Pamoja na kuchukiwa na watu wa nyumbani kwao kabisa tena ni ndugu wa damu waliozaliwa pamoja kwenye tumbo moja la mama na baba yao ni mmoja.Yusufu alichukiwa sana kwa sababu ya ndoto na tafsiri zake alizokuwa nazo kila mara akiota.

Kitu hicho hicho ambacho ndugu zake walikidharau na kuamua kumuuza kwa wafanyabiashara na kwenda kuwa mtumwa, Taifa la Misri lilimuona Yusufu bora kuliko watu wengine wowote katika nchi nzima, ndio maana Mfalme Farao anasema hadharani kabisa kuwa tupate wapi mtu kama huyu……

Mwanzo 41:37-44 

Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.

Nimekuwekea andiko lote upate picha kamili hapo mtu wa Mungu.

Suala sio tu kukataliwa na mazingira, suala ni kwamba hayo mazingira hayajui kile ulichokibeba ndani yako kwamba kinaweza kuwasaidia na wengine.

Aliyedharauliwa na kuuzwa kutoka nyumba ya Yakobo, akaonekana wa maana na wa thamani sana mbele ya farao na taifa zima, hata akapewa cheo cha waziri mkuu.

Sijui kama unaelewa njia za Mungu akitaka kumbariki na kumfanikisha mtu wake.

Anyway, tukutane Madhabahuni Youtube channel ya SIRI ZA BIBLIA nikufundishe zaidi na pia tufanye maombi ya pamoja kuombea mazingira tuliyonayo ili yasigeuke kuwa kikwazo kwa kufanikiwa kwako.

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA

Maarifa ya ki-Mungu

+255 758 708804


 SADAKA